Friday, March 29, 2019

Oktay Amepigwa Marafuku Na Caf

Kocha wa Gor mahia Hassan Oktay amepigwa marufuku ya kutohudhuria mechi yao ya mkondo wa  kwanza dhidi ya RS Berkane ya Morocco mnamo tarehe 7 Aprili.

Oktay alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuteta kupitia uamuzi wa refa kwenye mechi yao ya mwisho kwenye kundi D dhidi ya Pero Atletico ya Angola ugani  Kasarani wiki mbili zilizopita

Kocha huyo raia wa uturuki mwenye asilia ya Cyprus atakosa mechi hiyo ya robo fainali itakayandaliwa Nairobi huko akijiunga na wachezaji wake nahodha Harun Shakava, Ernest Wendo, Jacques Tuyisenge na Shafik Batambuze kwenye orodha ya waliopigwa marufuku kwenye timu hiyo.

Caf imethibitisha kwamba kocha huyo amepigwa marufuku na hatakubaliwa kukaa kando ya uwanja na pia harusiwa kuingia kwenye chumba cha kubadilisha nguo cha wachazeja wa Kogalo.

Shakava hatacheza mkondo wa kwanza kwa kuwa na kadi mbili za njano kwa mechi mbili tofauti huko Batambuze, Tuyisenge na Wendo wakikosa mkondo zote za robo fainali kwa kuonyeshwa kadi nyekundu.

Gor mahia watachuana na kariobangi sharks kwenye mechi ya KPL ugani Moi stadium Kisumu kuanzia saa tisa.

No comments:

Post a Comment

Emotions of the Game!

Football just like other sports brings a tidal of emotions and feelings when it happens.Its never a surprising scene to see a kid breakdown ...