Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba
wanawake ndio wahanga wakubwa wa ukatili wa jinsia.
Visa vya ukatili vimeongezeka humu
nchini katika siku za hivi karibuni, kutokana na kuongezeka kwa ripoti za mume
kumuua mkewe, mke kumuua mumewe au watoto kuuawa na baba au mama na hata watoto
kunajisiwa.
Ukatili husababishwa na mambo mengi,
ikiwemo kutoelewana, hasira, chuki, matatizo ya kifedha, kupoteza kazi, kutaka kuonekana
kudhibiti familia, na matumizi ya pombe na mihadarati.
Kwa mujibu wa Bibilia kwenye kitabu cha
Methali 15 moja, jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea
ghadhabu.
No comments:
Post a Comment