Friday, March 15, 2019

Chelsea Na Arsenal Kwenye Robo Fainali

Timu ya Chelsea iliadhibu Dynamo Kyiv kwa mabao tano kwa sufuri ugenini Olympic stadium.
 
Chelsea walionyesha mchezo nzuri kwenye mechi hiyo huko Mchezaji raia wa Ufaransa Oliver Giroud akicheka na wavu mara tatu na kuongeza idadi ya mabao zake msimu huu kwenye Eufa Europa league hadi tisa.
 
Marcos Alonso na Column Hudson Odoi pia walijiandikisha kwenye kitabu cha wafunga bao na kusaidia chelsea kufika  kwenye robo fainali ya kombe hilo wakiwa na mabao nane kutokana na ushindi wao ya mabao tatu kwenye mkondo wa kwanza stamford bridge. 
 
Vilevile,Timu ya Arsenal walishinda Rennes ugani emirates kwa mabao tatu kwa sufurina kujipa tiketi kwenye robo fainali ya kombe hilo.

Mchezaji raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang alifunga mabao mawili ya kwanza na ya mwisho huko Ainsley Maitland-Niles akifunga bao moja na kusaidia arsenali kulipiza kisasi baada ya kupoteza ugenini kwa mabao tatu kwa moja hivyo basi kushinda Rennes kwa idadi ya mabao.

Matokeo ya mechi zingine za  Europa zilizochezwa usiku wa Alhamisi ni pamoja na
 
Krasnodar walitoka sare ya moja kwa moja dhidi ya valencia.
Salzburg walipiga napoli kwa mabao 3 kwa moja.
Benfika wakapiga Dinamo Zagreb kwa mabao tatu kwa sufuri.
Internazionale ilipigwa na Eintracht Frankfurt nyumbani kwao kwa bao moja kwa sufuri.
Slavia Praha wakashinda Sevilla kwa mabao manne kwa tatu.
Villareal walishinda Zenit kwa mabao mawili kwa sufuri.

No comments:

Post a Comment

Emotions of the Game!

Football just like other sports brings a tidal of emotions and feelings when it happens.Its never a surprising scene to see a kid breakdown ...