Thursday, March 14, 2019

Kogalo waadhibu Homeboyz

Timu ya Gor Mahia almaarufu Kogalo, imeshinda vijana wa Kakamega homeboyz kwa mabao mawili kwa moja kwenye mechi ya kung'ang'ania taji la kombe la klabu bingwa nchini KPL.

Mechi hiyo imechezwa ugani Machakos kuanzia saa kumi alasiri.

Vijana wa Homeboyz ndiyo waliotangulia kufunga kupitia mchezaji wao Luke Namanda mnamo dakika 51.

Kogalo walilipiza mnamo dakika ya 67 kupitia mguu yake Francis Mustafa kabla ya kuongeza ya pili na ya ushindi dakika mbili baadaye kupitia Boniface Owino Omondi.

Kumbuka Kogalo walifanya mabadiliko ya watu kumi kwenye squadi yao ili kujiandaa kwa mechi dhidi ya klabu ya petro jumapili.

Gor mahia wanahitaji ushindi wowote ili kufika kwenye robo fainali ya kombe la CAF confedaration.

No comments:

Post a Comment

Emotions of the Game!

Football just like other sports brings a tidal of emotions and feelings when it happens.Its never a surprising scene to see a kid breakdown ...