Tuesday, March 19, 2019

Kongamano La Kimataifa Kisumu

Governor wa Kisumu Profesa Peter Anyang' Nyong'o  amefungua rasmi kongamano la kimataifa kuhusu makazi ya kutosha na gharama ya chini.

kongomano hilo ambayo imepangwa na shirika la Grassroot Trust ikiungana na kaunti ya Kisumu imeng'oa nanga hivi leo hadi siku ya Alhamisi ambapo inatarajiwa kufungwa rasmi na Mheshimiwa Raila Odinga.

Akizungumza kwenye kongamano hilo Nyong'o amesema kuwa wanaendeleza mipango za kuimarisha makazi jijini kisumu wakiungana na mashirika zisizo za serikali ili kuhakikisha kwamba wakazi wa kisumu wanaishi kwa nyumba zenye gharama za chini,zenye usalama na maji,na vituo vya afya.

Wageni wengi kutoka ugaibunu pamoja na wakazi wa kisumu wamehudhuria kongomano hilo inayofanyika kwenye hoteli ya kifahari ya Grand Royal Swiss iliyoko eneo ya Riat jijini Kisumu .
 
Lawrence Apiyo ambaye ni mshirikishi wa shirika la Grassroot trust akizungumza amesema kwamba wanafanya juhudi kama shirika kuhakikisha wakazi wa kisumu wanaishi kwa nyumba nzuri.

No comments:

Post a Comment

Emotions of the Game!

Football just like other sports brings a tidal of emotions and feelings when it happens.Its never a surprising scene to see a kid breakdown ...