Tuesday, March 26, 2019

''Unapanga Basi Nyuma Kama Mourinho!''Van Gaal Asema.

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal amesema hapendezwi na mbinu za kaimu wa manchester united Ole Gunnar Solskjaer.

Van Gaal ambaye alifutwa kazi Manchester na mahali pake kuchukuliwa na Jose Mourinho amesema kwamba Kocha huyo msimamizi raia wa Norwey anacheza mchezo wa kujihami sana nyuma kama alivyofanya Mourinho.

Mourinho alifaamika sana na mbinu yake ya ''kupanga basi nyuma'' na kutumia mashambulizi ya kushtukiza ili kupata ushindi.

Ingawa Manchester walishindwa na Arsenal kwenye mechi ya premier Uingereza mtawaliwa na pia kupoteza dhidi ya wolves kwenye kombe la FA ,Ole Gunnar Solskjaer ameongoza vizuri sana timu hiyo tangu achukue ushukani toka kwa Mourinho mwezi disemba huko akifikisha manchester united kwenye robo fainali za mechi za klabu bora EUFA na kuwapandisha hadi nafasi ya nne bora kwenye jedwali ya ligi kuu Uingereza.

Van Gaal pia amesema kwamba kocha huyo kama vile Mourinho hapatii vijana wadogonafasi ya kucheza kama alivyofanya yeye akiwa kocha manchester mwaka wa 2014 na 2016.


No comments:

Post a Comment

Emotions of the Game!

Football just like other sports brings a tidal of emotions and feelings when it happens.Its never a surprising scene to see a kid breakdown ...