Timu ya Manchester United walionyesha mchezo mzuri usiku wa jumatano na kuishinda timu ya PSG kwa kile watu wengi wanaita kama miujiza.
Kumbuka Man United walienda kwenye hiyo mechi wakiwa nyuma kwa mabao mawili kutokana na kushindwa nyumbani na PSG kwa mkondo wa kwanza kwenye kombe la EUFA wiki mbili zilizopita.
Vijana wa PSG waliitaji sare lolote ili kujipa tiketi kwenye robo fainali lakini vijana wa Manchester chini ya kocha msimamizi Ole Gunnar Solskjaer walikuwa na mipango nyingine.
Mbelgiji Romelu Lukaku ndiye aliyetangulia kufunga bao la kwanza dakika mbili tu za mchezo lakini wanaPSG wakasawazisha dakika kumi baadaye na kuvunja moyo ya Manchester.
Ganga ganga za Lukaku iliwapa Manchester matumaini alipofunga bao la pili mnamo dakika ya 30 kabla ya Marcos Rashford kufunga kupitia tuta la penalti dakika za mwisho na kubandua psg kutoka kwenye mashindano hayo.
Penalti hiyo ya manchester imeleta hisia mbalimbali baina ya makocha na wachezaji mbalimbali;Neymar Jr ambaye hakuchezea PSG jana usiku kutokana na majeraha alikasirishwa sana na huo uamuzi na kusema kwamba penalti haikufaa.
Neymar ameandika kwenye twitter ya kwamba waamuzi wa mechi hiyo hawakujua walichukuwa wakifanya na hakuelewa walichokiona kwenye VAR .
Hayo yote tisa,kumi ni aty Manchester wako kwenye robo fainali.
No comments:
Post a Comment