Timu ya Manchester united imempea kocha Ole Gunnar Solskjaer kandarasi ya kuwa meneja mkuu Old traford kwa miaka tatu zijazo.
Kocha huyo raia wa Norwey amekuwa kaimu wa mancester tangu disemba baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi..
Kocha huyo raia wa Norwey amekuwa kaimu wa mancester tangu disemba baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi..
Solskjaer ameonyesha huongozi nzuri sana huko akishinda mechi kumi na nne kati ya mechi zote kumi na tisa aliongoza kama kocha wa Manchester na pia kuwafikisha kwenye robo fainali ya kombe la klabu bingwa Eufa.
Kocha huyo ameiletea wachezaji wa Manchester morale na kuwapa motisha tangu achukue ushukani na kuwapeleka hadi nafasi ya nne kwenye jedwali ya kombe la uingereza-EPL.
Naibu mwenye kiti mkuu wa Manchester Ed Woodward amesema kwamba anaamini kuwa Ole gunnar ndiye mkufunzi nzuri kwa Manchester kwa hivi sasa na kwa siku za usoni.
Aliongeza kuwa tangu Solskjaer kuingia Manchester mwezi disemba ameleta matokeo nzuri na za kufurahisha mashabiki na bodi ya timu nzima,kwa hivyo anjua atapeleka Manchester kushinda taji mbalimbali.
Akizungumza baada ya kupewa kazi ,Ole amesema kwamba amekuwa na ndoto ya kuwa kama meneja wa Manchester kwa muda sasa ,kwa hivyo amejazwa na furaha tle na ako tayari kuongoza Manchester kushinda mataji.
No comments:
Post a Comment