Monday, March 11, 2019

Bora Nyumba! ama Nyumba Bora?

Nyumba na makazi bora ni mojawapo kati ya agenda nne kuu za rais Uhuru Kenyatta...


Lakini wakenye wengi bado wanaishi kwenye nyumba duni zenye mazigira chafu,kukosa maji,kutokuwa na hospitali,ukosefu wa usalama na mashida zinginezo.
Nilipotembea mtaani Bandani iliyoko jijini Kisumu tulisuhudia baadhi ya nyumba ambazo hali zao si nzuri kwa afya ya binadamu yeyote yule.Baadhi ya nyumba hizo hazina hata vyoo kwa hivyo  wanaoishi huko wanahatarisha maisha yao kwa kulipa pesa kiasi.
Nilipozungumza na kikundi cha project comitee management{pmc}ambao wanafanya juhudi na mradi ya ujenzi wa nyumba za matofali ili angalua kuinua hali ya maisha ya wanaoishi Bandani wamesema chama yao inalenga kuhakikisha  kwamba wakazi wa Bandani wanaishi kwa nyumba bora  kwa siku za usoni.
 
Mwenyekiti wa PMC Bwana Abubakar Hasan Makengeza amesema kuwa serikali ya kaunti ya kisumu imewapa machine ya kutengeneza matofali kwa hivyo wao hutengeneza takriban matofali alfu moja kwa siku.
Ameongeza kwamba wako na kamati ya watu sita ambao wanongeza kikundi cha kuhakikisha kwamba wakazi wa bandani wataishi kwa nyumba nzuri.



No comments:

Post a Comment

Emotions of the Game!

Football just like other sports brings a tidal of emotions and feelings when it happens.Its never a surprising scene to see a kid breakdown ...