Siku Ya Misitu Kimataifa
Wakazi wa kisumu wameungana na ulimwengu leo hii kuidhimisha siku ya misitu.
Sherehe hiyo iliandaliwa kwenye mlima wa kajulu iliyoko kisumu. Viongozi hao walianza na kupanda miti kabla ya kuhotubiawakaziwa eneo hilo.
Akizungumza kwenye sherehe hiyo Waziri wa maji, mazingira na mali asilimia kaunti ya Kisumu Salmon Orimba amesema kwamba serikali ya kaunti ya Kisumu imeekeza milioni 20 katika zoezi la kuimarisha mazingira ikiwemo upanzi wa miti ili kuhakikisha wanaongeza sehemu ya miti kutoka asilimia 0.4 hadi asilimia 10 kufikia mwaka 2022.
Kaunti ya kisumu inashikilia nafasi ya 46 huko ikishinda Kaunti ya Siaya pekee yake.
Sherehe kama hiyo iliandaliwa Siaya kaunti ambao wanashika mkia kwa upanzi wa miti.
No comments:
Post a Comment