Monday, April 1, 2019

Gor Mahia yazidi kunawiri ligini

Miamba wa soka nchini Gor Mahia wamepanua mwanya wa alama tano kileleni kwa jedwali la ligi kuu ya soka nchini – KPL, kufuatia ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Nzoia Sugar ugani Moi jijini Kisumu.
 
Hansel Ochieng aliiweka Nzoia Sugar kifua mbele, kabla ya Francis Mustapha kuisawazishia Gor Mahia.
Mabao hayo mawili yalifungwa kabla ya dakika ya kumi huku Geoffrey Ochieng akiifungia Gor Mahia bao la ushindi, dakika za mwisho kabisa za mchezo huo.
Kocha mkuu wa Gor Mahia Hassan Oktay, ameonyesha kufurahishwa na matokeo hayo.
Naye kocha mkuu Nzoia Sugar FC Vincent Situma, ameelezea kufarahishwa na juhudi za wachezaji wake licha ya kupoteza dhidi ya Gor Mahia.
Gor Mahia inaongoza jedwali la KPL kwa alama 41, alama tano mbele ya nambari mbili Sofapaka. Miamba hao watachuana na Sony Sugar ugani Moi jijini Kisumu siku ya Jumatano.


No comments:

Post a Comment

Emotions of the Game!

Football just like other sports brings a tidal of emotions and feelings when it happens.Its never a surprising scene to see a kid breakdown ...