Thursday, April 4, 2019

Mechi za KPL

Mechi tatu za ligi kuu ya soka nchini-KPL,zimechezwa hivi leo.

Kariobangi Sharks wametoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya zoo kericho kwenye uga wa Nairobi City.

Sofapaka nao pia wametoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Vihiga United kwenye uga wa Nyao jijini nairobi.

Nzoia sugar wametesa nyasi bure dhidi ya posta rangers na kutoka na sare ya kutokuwa na bao kwenye uga wa Masinde Muliro BUngoma.

Huko AFC Leopards almaarufu Ingwe wakishinda Chemelil Sugar kwa mabao mawili kwa sufuri kwenye uga wa Nyanyo jijini Nairobi.

Wednesday, April 3, 2019

Gor Mahia Watozwa Faini Ya Shilingi 906,000


Gor Mahia watalazimishwa kulipa faini kubwa baada ya kupatikana na hatia kwa kosa iliyowakabili kutokana na mashabiki kuzua vurugu kwa mechi yao dhidi ya AFC Leopards na KCB .
 
Mbele ya kamati huru ya malalamishi na nidhamu, Independent Disciplinary & Complaints Committee (IDCC),Kogalo wametozwa faini ya shilingi za kenya alfu 606,000 kwa vitendo vya ukosefu wa nidhamu kwa mechi yao dhidi ya KCB mnamo tarere 27 mwezi January mwaka 2018 kwa mashtaka ya kwanza.

Gor mahia vilevile imetozwa faini na kamati hiyo huru ya shilingi za Kenya alfu 300 kwa makosa hayo hayo dhidi ya AFC Leopards mnamo tarehe 25 mwezi Agosti mwaka jana.

Timu hiyo imepewa nafasi ya siku sitini kulipa hela izo zote za Kenya alfu 906,000 .


Tuesday, April 2, 2019

Pendekezo La Kupunguza Umri Ya Kufanya Mapenzi Kwa Hiari

Baadhi ya Viongozi katika kaunti ya Kakamega,wamekosoa pendekezo la baadhi ya majaji kua umri wa kufanya mapenzi kwa hiari upunguzwe kutoka miaka 18 ya sasa hadi miaka 16.

Akiongea na wanahabari mjini kakamega,seneta wa kaunti hiyo Cleophas malala amesema kuwa pendekezo hilo kamwe haitasaidia kupunguza visa vya mimba za mapema,miongoni mwa watoto wa kike humu nchini.

Kauli yake iliungwa mkono na mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kakamega Elsie Muhanda.

Je ni umri gani watu wanapaswa kushiriki kwenye mahusiano ya kingono kwa hiari?

Monday, April 1, 2019

Gor Mahia yazidi kunawiri ligini

Miamba wa soka nchini Gor Mahia wamepanua mwanya wa alama tano kileleni kwa jedwali la ligi kuu ya soka nchini – KPL, kufuatia ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Nzoia Sugar ugani Moi jijini Kisumu.
 
Hansel Ochieng aliiweka Nzoia Sugar kifua mbele, kabla ya Francis Mustapha kuisawazishia Gor Mahia.
Mabao hayo mawili yalifungwa kabla ya dakika ya kumi huku Geoffrey Ochieng akiifungia Gor Mahia bao la ushindi, dakika za mwisho kabisa za mchezo huo.
Kocha mkuu wa Gor Mahia Hassan Oktay, ameonyesha kufurahishwa na matokeo hayo.
Naye kocha mkuu Nzoia Sugar FC Vincent Situma, ameelezea kufarahishwa na juhudi za wachezaji wake licha ya kupoteza dhidi ya Gor Mahia.
Gor Mahia inaongoza jedwali la KPL kwa alama 41, alama tano mbele ya nambari mbili Sofapaka. Miamba hao watachuana na Sony Sugar ugani Moi jijini Kisumu siku ya Jumatano.


Emotions of the Game!

Football just like other sports brings a tidal of emotions and feelings when it happens.Its never a surprising scene to see a kid breakdown ...