Friday, March 5, 2021

Si ASA!

"Siasa ni mchezo mchafu".
Vuta nikuvute ilishuhudiwa hapo jana kwenye maeneo mbali mbali nchini ambapo uchaguzi mdogo uliandaliwa. 
Si wanasiasa, si wananchi, si polisi, kila mmoja akijipata katika mchezo huu mchafu.
Kwa kweli fahali wawili wapiganapo nyasi ndizo huumia.
Wanahabari wanne walipelekwa hospitalini kuuguza majeraha waliyopata kutokana na rabsha na vita vilivyotokea kwenye vituo vya kupiga kura.
Cha kusikitisha mno ni kwamba hata viongozi wetu wanaofaa kuwa vielelezo walionekana wakishikana mashati huku waking'ang'ania kura.
Wengine wao hata wakaamua kuvamia maajenti wa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi (IEBC).Aliyekuwa waziri wa mchezo nchini Rashid Echesa alionekana akimzaba kofi mmoja wa maajenti wa IEBC baada ya kutofautiana kuhusu jambo fulani. Je huu ni ungwana? Polisi walilazimika kutumia vitoa machozi ili kuwatimua walioleta fujo; japo  kunao waliotumia vibaya uwezo waliopewa kwa kuwanyanyasa na kuwakandamiza wananchi.
Polisi wengine walitumia nguvu nyingi kupata kiasi kuwapiga na hata kuwaumiza watu bure.
Mbona tuumizane?, mbona tupigane?.Ni nini chanzo cha vita ivi vya kisiasa?
1.kutoamini tume ya uchaguzi nchini IEBC
Ni dhahiri shahiri kwamba viongozi wengi na hata wananchi hawana imani na tume ya uchaguzi hapa nchini. Ndo maana wanaamua kuleta virugo ili kuwatisha angalau waogopwe ndo washinde.
2.uvamizi wa uchaguzi
Wananchi na wanasiasa wamekuwa wakilalamika kila uchao tunapokuwa na uchaguzi kuhusu uvamizi na kuibwa kwa kura.
3.kupea wapinzani uoga
Viongozi wengine wanaamua kuleta vita na vitisho ili kujaza wapinzani wao na uoga. Wanawatisha wenzao huko wakiamini kwamba wengine uhenda wakaogopa hata kujitokeza kupiga kura na hivyo basi faida kwao. 
4.vijana kukubali kutumia vibaya
Vijana wengi wanakosa ajira nchini, hivyo basi wanajipata kwenye kazi ambao si nzuri bora wapate pesa. Wanasiasa wanatumia hawa vijana vibaya kwa kuwapea pesa kidogo cha haraka ili walete virugo kwenye vituo vya kupiga kura.
5.Viongozi kutoheshima sheria
Viongozi wengine wanadhani wako juu ya sheria kwa kuwa wanapesa. Kwa mfano, aliyekuwa waziri wa mchezo Echesa anapoamua kupiga afisa wa IEBC anaamini kwamba hakuna kitu atafanyiwa na sheria kwa kuwa ako na pesa. Anaamini kwamba hata akishikwa na polisi atatoa pesa na ataachiliwa.
6.Ufisadi
Ufisadi ni ugonjwa mbaya sana kushinda hata Corona. Wananchi wengine hata hawatokei kupiga kura kwa kuwa wanajua hata wakipiga kura bado kutakuwa na ufisadi kwa hivyo kura zao hazitakuwa na maana.

Huu ni kilio cha haki.

No comments:

Post a Comment

Emotions of the Game!

Football just like other sports brings a tidal of emotions and feelings when it happens.Its never a surprising scene to see a kid breakdown ...