Sunday, June 21, 2020
SIKU YA BABA ULIMWENGUNI
Wakenya waliungana na walimwengu kusheherekea siku ya baba ulimwengu jumapili 21.
Picha za akina baba zilikuwa kote mtandaoni haswa kwenye mtandao za kijamii kama vile facebook, whatsup na hata Twitter.
Kila mtu alionekana kumpenda baba huko wakiwapongeza kwa maneno matamu.
Lakini swali ni kwamba, je unachukua wakati wako kukaa na baba?,kuzungumza naye?, kumwonyesha unampenda?.
Ama ni haya mapenzi ya mtandao? ya kuonyesha jamaa na marafiki kwamba unampenda baba?lakini ukweli ni kwamba hata mwezi unapita kabla kumjulia hali nyumbani?
Akina baba mara nyingi husaulika sana, si kama akina mama. Ni mara nyingi sana tunasherehekea siku za akina mama duniani uko tukiwatumia pesa kuwaonyesha mapenzi yetu.
Lakini tunawasahau baba.
Baba ana majukumu mengi sana katika familia na hivyo basi tunafaa kumwonyesha mapenzi yote na kumpongeza kila tunapopata nafasi.
Ni dhahiri shairi kwamba kuna wazazi wengi sana haswa wa kiume ambao ni wazazi tu ila si baba. Kuwa mzazi ni tofauti sana na kuwa baba.
Unakuwa mzazi unapozaa tu mtoto lakini unakuwa baba unapotimiza mahitaji za mtoto huyo uliye mzaa.
Sifa za baba
*mwenye upendo kwa watoto
*Mwenye kujali watoto wake
*Baba mcheshi anaeweza kucheza na watoto wake japo hii inategemea maana kuna wababa uso wa mbuzi hao.
*Baba mwenye mawasiliano mazuri na watoto wake
*Baba mwenye subira na mvumilivu
*Baba muelewa
*Baba rafiki wa watoto
*Baba mwenye muda na nafasi ya kukaa na watoto wake kuwasikiliza.
*Baba mtafutaji na naetunza familia yake kwa kuwapa watoto wake mahitaji yao
*Baba mwaminifu
*Baba mlinzi na mhimili mkuu wa familia na watoto wake.
*Baba anaewajibika kutatua matatizo ya familia kwa hekima na busara.
*Baba anaempenda na kumuheshimu mama wa watoto wake(mkewe).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Emotions of the Game!
Football just like other sports brings a tidal of emotions and feelings when it happens.Its never a surprising scene to see a kid breakdown ...

-
Nyumba na makazi bora ni mojawapo kati ya agenda nne kuu za rais Uhuru Kenyatta... Lakini wakenye wengi bado wanaishi kwenye nyumba du...
-
Timu ya Manchester United walionyesha mchezo mzuri usiku wa jumatano na kuishinda timu ya PSG kwa kile watu wengi wanaita kama miujiza. ...
No comments:
Post a Comment